Utundu wa makanga SuperMetro

  • | Citizen TV
    206 views

    Familia ya Gilbert Thuku Kimani jamaa aliyefariki baada ya kusukumwa kutoka kwa gari la kampuni ya super metro katika barabara ya thika inataka polisi kufanya uchunguzi wa kina. Tayari polisi wanasema wamemtia mbaroni dereva wa gari lililohusika na tukio hilo na wanamsaka makanga anayedaiwa kumsukuma Gilbert na kusababisha kifo chake. Marehemu alikosa shilingi 30 tu za kuongezea kwenye nauli yake na hiyo ikawa sababu ya kusukumwa kutoka kwa gari hilo na kufariki...