Zaidi ya watu milioni 1.3 wanaishi na virusi vya HIV nchini Kenya

  • | K24 Video
    12 views

    Zaidi ya watu milioni 1.3 wanaishi na virusi vya HIV nchini Kenya, na safari yao—kutoka kwa wahudumu wa afya waliojitolea kuokoa maisha hadi kwa wale wanaopambana na changamoto zao binafsi—imekuwa ngumu kwa mwezi mmoja sasa tangu serikali ya marekani ilipotoa agizo la kusitisha ufadhili kwa siku 90. Wiki hii, serikali ya kitaifa na za kaunti zilifanya mkutano wa mashauriano ili kutafuta mbinu za kufadhili mipango ya HIV kupitia ufadhili wa ndani ili kuepuka janga linalonyemelea.