Mzozo wa Sudan wazidi kutokota, katika Dira ya dunia TV

  • | BBC Swahili
    630 views
    Mapigano yanaendelea nchini Sudan kwa ajili ya udhibiti wa mji mkuu Khartoum na viunga vyake. Vikosi vya Rapid Support Forces vilishambulia eneo la Omdurman, mji pacha wa mji mkuu, na kuua raia sita, ikiwa ni pamoja na watoto wawili. Kwa mujibu wa mamlaka ya eneo hilo, shambulio hilo la bomu la hapo jana lilipiga maeneo ya makaazi, na kuwalenga raia ndani ya nyumba zao sambamba na watoto ambao walikua wakicheza nje.