Kukomesha malaria : Kaunti ya Busia yaimarisha mikakati

  • | KBC Video
    4 views

    Serikali ya kitaifa kwa ushirikianao na serikali ya kaunti ya Busia imeimarisha juhudi za kukabiliana na ugonjwa wa malaria katika maeneo chepechepe na misitu kwa kutumia droni kunyunyiza dawa za kuangamiza viluilui. Akiongea wakati wa uzinduzi wa awamu ya tatu ya kampeni ya kukabiliana na ugonjwa wa Malaria katika kaunti ya BusiaDkt Willis Akhwale ambaye ni katibu wa baraza la kitaifa la kudhibiti ugonjwa wa Malaria alisisitiza kuwa changamoto kuu zinazosibu kaunti ya Busia ni uwepo wa eneo chepechepe na chemi chemi nyingi za maji ambazo zinachangia ongezeko la visa vya ugonjwa wa Malaria. Alisema kuwa teknnolojia ya droni tayari imepiga hatua katika kupunguza visa vya ugonjwa huo. Dkt Akhwale pia alihimiza wakazi kushiriki katika vita dhidi ya ugonjwa wa malaria kwa kutumia neti zilizowekwa dawa na kutafuta usaidizi wa matibabu iwapo wataambukizwa

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive