Huduma za serikali : Watu walio na ulemavu watakiwa kujisajili

  • | KBC Video
    4 views

    Mbunge wa Busia Catherine Omanyo ameitaka serikali kuu kupitia idara ya Huduma za Jamii kuanzisha kampeni za uhamasisho kwa watu walio na ulemavu kuhakikisha wanajisajili kikamilifu ili wanufaike na huduma za serikali pamoja na ruzuku nyinginezo. Akizungumza katika eneo la Apatit wakati wa uzinduzi wa mpango wa ugawaji viti 100 vya magurudumu kwa watu wlio na ulemavu, Omanyo alikariri kuwa walemavu wengi wametengwa na familia zao kwani wanachukuliwa kuwa mzigo, hatua inayowanyima haki zao za kimsingi. Wakazi walipongeza hatua hiyo wakisema itawapa walemavu fursa ya kujiendeleza katika jamii.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive