Watu sita wameuawa na wanne kujeruhiwa kufuatia shambulio la kigaidi kwenye kambi ya polisi Garissa

  • | K24 Video
    1,658 views

    Watu sita wameuawa na wanne kujeruhiwa kufuatia shambulio la kigaidi kwenye kambi ya polisi katika kaunti ya Garissa, iliyoko mashariki mwa kenya karibu na mpaka wa Somalia. Shambulio hilo lilitokea mapema asubuhi ya jumapili, majira ya saa 11 alfajiri, katika kambi ya hifadhi ya polisi ya kitaifa eneo la Biyamadhow, Wilayani Gafi.