Kaunti ya Kwale yazindua bwawa la maji ili kukomesha njaa

  • | KBC Video
    12 views

    Ni afueni kwa wakazi wa kaunti ndogo za Kinango na Lungalunga baada ya serikali ya kaunti ya Kwale kuzindua bwawa la maji litakalohudumia maeneo hayo. Gavana wa kaunti ya Kwale Fatuma Achani amesema serikali ya kaunti hiyo inanuia kutatua suala la uhaba wa chakula katika eneo hilo, akisisitiza kwamba kipaumbele kitapewa maeneo kame ya Kinango, Samburu na Lungalunga. Wakazi wa kaunti hizo ndogo wamekuwa wakikabiliwa na tatizo la njaa kwa miongo mingi kutokana na hali duni ya anga ambayo huathiri uzalishaji chakula.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive