Viongozi wa wanawake Trans Nzoia wataka afya ya mama na mtoto izingatiwe

  • | Citizen TV
    169 views

    Muungano wa viongozi wanawake katika Kaunti ya Trans Nzoia umetaka hatua za haraka kuchukuliwa ili kuhakikisha kuwa hakuna mama anayepoteza maisha wakati wa kujifungua.

    Katika warsha iliyohudhuriwa na wanahabari na wadau kutoka sekta mbalimbali wakiwemo watetezi wa haki za binadamu, muungano huo ulieleza masikitiko yao kuhusu vifo vya kina mama hospitalini.. Walitoa wito kwa serikali na mamlaka husika kuongeza idadi ya wahudumu wa afya, kuhakikisha upatikanaji wa damu ya kutosha, dawa , na vifaa vya matibabu hasa katika vitengo vya afya ya uzazi na watoto.