Watu tisa wafariki kwenye ajali barabarani

  • | KBC Video
    399 views

    Watu tisa wamethibitishwa kufariki katika visa viwili tofauti vya ajali barabarani vilivyotokea katika kaunti za Kiambu na Kirinyaga. Katika tukio la kwanza,watu saba waliangamia baada ya matatu inayomilikiwa na chama cha ushirika cha Kijabe Line yenye uwezo wa kuwamudu abiria-14 kubingiria mara kadhaa katika makutano ya barabara ya Kamandura kwenye barabara kuu ya Nairobi-Nakuru baada ya dereva kupoteza mwelekeo leo asubuhi huku wengine wawili wakifariki jana usiku katika kisa cha pili baada ya gari walimokuwa wakisafiria kutumbukia kwenye mto Nyamindi katika daraja la Kaboro,eneo bunge la Gichugu,kaunti ya Kirinyaga . Mwanahabari wetu Timothy Kipnusu ana maelezo zaidi.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive