Wakazi wa Bonde la Ufa Wapinga Usimamizi wa Misitu Kupewa Watu Binafsi

  • | K24 Video
    80 views

    Wakazi kutoka kaunti za kaskazini mwa Bonde la Ufa wamepinga vikali mapendekezo ya Shirika la Huduma za Misitu (KFS) yanayolenga kuweka usimamizi wa misitu ya umma mikononi mwa watu binafsi. Wakiongozwa na miungano ya kijamii ya misitu (CFA), wakazi waliotoa maoni yao katika kikao cha umma kilichofanyika Eldoret waliitaka Wizara ya Mazingira kufutilia mbali pendekezo hilo. Wanasema hatua hiyo inaweza kufungua mlango kwa watu binafsi kumiliki misitu ya umma kwa njia za ujanja na kuchochea unyakuzi wa ardhi.