Kwa nini CHADEMA imetupwa nje ya uchaguzi mkuu Tanzania?

  • | BBC Swahili
    43,375 views
    Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, CHADEMA, kimezuiwa kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka huu, siku chache baada ya kiongozi wake kufunguliwa mashtaka ya uhaini. Mkurugenzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ramadhani Kailima, amesema CHADEMA imeshindwa kusaini hati ya maadili iliyotakiwa kufanyika Jumamosi, hivyo kumaanisha kuwa chama hicho kimeondolewa kwenye uchaguzi wa Oktoba.