Tusker kileleni mwa ligi kuu baada ya kuilaza Nairobi City Stars

  • | Citizen TV
    262 views

    Tusker FC imepanda kileleni mwa ligi kuu nchini baada ya kuilaza nairobi city stars kwenye mechi iliyochezwa uwanjani Kenyatta kaunti ya Machakos. Bidco nao walijikwamua kutoka kwenye hatari ya kushushwa ligi kwa ushindi wa mbili bila dhidi ya mathare united. Clinton Osiago alipachika bao la kwanza dakika 25 kabla ya abuko simon kuongeza la pili dakika kumi kabla ya mapumziko. Kwenye mechi nyengine muranga seal na kariobangi sharks walikabana sare tasa huku shabana wakiinyeshea talanta mabao manne kwa mawili.