Mwakilishi wadi ya Dela-Anole Yussuf Hussein arejea nyumbani

  • | Citizen TV
    773 views

    Ilikuwa siku ya shangwe na furaha katika Kaunti ya Wajir wakati mwakilishi Wadi ya Dela-Anole Yussuf Hussein, aliyekuwa ametekwa nyara, aliporejea nyumbani kwa bashasha. Umati wa watu ulijitokeza kwa wingi mitaani wakiimba na kupiga vigelegele Kwa kusherehekea kurejea kwake kwa furaha kana kwamba ni mwana wao aliyepotea kwa muda mrefu. Akiwa ameandamana na Mbunge wa Eldas, Aden Keynan, MCA huyo alipokelewa kwa hisia tele