Watu wawili wamefariki dunia huku wengine watano wakiachwa katika hali mahututi katika kituo cha afya huko Maua, Kaunti ya Meru, baada ya kunywa pombe haramu. Vifo hivyo vimezua taharuki katika eneo hilo, huku wakazi wakilaumu watawala wa serikali kwa madai ya kuidhinisha biashara ya pombe haramu baada ya kupokea hongo kutoka kwa watengenezaji wa pombe hiyo, hali ambayo inahatarisha maisha ya waraibu.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive