- 343 viewsDuration: 2:50Tume ya uchaguzi nchini IEBC imeonya dhidi ya ukiukaji wa sheria za uchaguzi kabla, wakati na baada ya uchaguzi mdogo Alhamisi Ijayo katika maeneo mbali mbali nchini. Kamishna wa tume hiyo Mohammed Hassan Nur ambaye alisimamia zoezi la kusambaza vifaa vya kupiga kura, aliwahakikishia wapiga kura na maafisa wa IEBC usalama wao kufuatia mkutano maalum wa tume hiyo na inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja