Wataalamu wa afya humu nchini wanaonya kuwa juhudi za kukabili ugonjwa wa Ukimwi zinakabiliwa na tishio jipya baada ya maambukizi mapya ya ukimwi elfu-20 na vifo elfu-21 vinavyohusiana na ugonjwa huo kunakiliwa humu nchini mwaka 2024. Akiongea jijini Nairobi kabla ya kuandaliwa kwa maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani mwaka huu, afisa mkuu mtendaji wa baraza la kitaifa la magonjwa ya kuambukiza Douglas Bosire alisema lazima taifa hili liwape kipa umbele watoto wanaobaleghe, vijana na kina mama ili kufanikiwa kukomesha ugonjwa wa UKIMWI kufikia mwaka 2030.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive