Skip to main content
Skip to main content

Homa Bay yakabiliwa na migawanyiko ndani ya ODM huku chaguzi ndogo zikikaribia

  • | KBC Video
    339 views
    Duration: 3:45
    Taswira ya kisiasa inakabiliwa na msisimko mkubwa huku chaguzi ndogo za juma lijalo zikizua kampeni kali, wengine wakiwaunga mkono wapinzani na wengine kubishana hadharani katika maeneo kadhaa. Kuanzia magharibni mwa nchi ambako waziri mwenye mamlaka makuu Musalia Mudavadi anatekeleza kampeni kukusanya pamoja kura ya jamii ya Luhya huku akitoa wito wa umoja na kuihimiza jamii hiyo kuunga mkono ajenda ya maendeleo ya serikali huku akiwaonya viongozi anaowashtumu kwa kuleta migawanyiko. Na huko Nyanza, mzozo mkubwa umezuka katika kaunti ya Homa Bay ambako gavana Gladys Wanga na naibu wake Oyugi Magwanga wanawaunga mkono wagombea hasimu kwenye kinyang’anyiro cha Kasipul na kubainisha migawanyiko katika chama cha ODM siku chache tu kabla ya kura hiyo huku viongozi wa upinzani wakikita kambi huko Ugunja kumpigia debe mgombea wao. Mwanahabari wetu Ben Chumba anatuarifu zaidi. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive