- 841 viewsDuration: 1:40Ubabe wa Kisiasa katika kampeni za uchaguzi mdogo Mbeere North huko Embu umeendelea huku serikali na upinzani wakilaumiana kwa tuhuma za kupangwa kwa vurugu siku ya uchaguzi. Aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua amedai kwamba kuna njama ya kuwatisha wakazi wa Mbeere North siku ya uchaguzi huku Naibu Rais Kithure Kindiki akidai kwamba Gachagua ana njama ya kugawanya jamii ya Mbeere.