Karata za kisiasa zilisheheni kwenye kinyang’anyiro cha ubunge wa Malava hivi leo baada ya mgombea wa chama cha DNA Joab Manyasi, kujiondoa na kumuunga mkono mgombezi wa chama tawala cha UDA, David Ndakwa. Hatahivyo, katika kujibu madai hayo, chama chake kilitangaza kwamba kilikuwa kimeondoa uwaniaji wake na kumuunga mkono mgombezi wa muungano wa upinzani, Seth Panyako. Haya yanajiri huku zikiwa zimesalia siku tatu pekee kabla ya kuandaliwa kwa uchaguzi mdogo wenye ushindani mkali tarehe 27, mwezi huu.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive