Mahakama kuu yabatilisha ushindi wa mbunge wa Lagdera Abdikadir Hussein Mohamed

  • | Citizen TV
    2,337 views

    Mahakama kuu imabatilisha ushindi wa mbunge wa Lagdera Abdikadir Hussein Mohamed. Mohamed, ambaye aliwania kiti hicho kwa tiketi ya chama cha ODM, ndiye mbunge wa kwanza ambaye uchaguzi wake umefutiliwa mbali. Mohammed alitangazwa mshindi kwa kupata kura 5,939 kwenye uchaguzi wa Agosti mwaka jana na kumbwaga Abdiqani Zeitun wa chama cha UDA aliyepata kura 4,863. Mohamed amesema atakata rufaa mahakamani.