Seli mundu: Adui mwilini mwangu

  • | BBC Swahili
    393 views
    Akiwa na umri wa miezi sita tu, Leah Kilenga aligundulika kuwa na seli mundu ‘sick-le cell’. Wazazi wa Leah waliambiwa na madaktari kwamba mtoto wao hatoweza kufika umri wa ujana wake. Badala yake amekuwa kinara wa matumaini kwa wagonjwa wa seli mundu nchini Kenya na kote barani Afrika, akipambana na unyanyapaa unaozunguka ugonjwa huo na mamlaka zinazoshindwa kutoa huduma za kutosha kwa wagonjwa wa seli mundu. #bbcswahili #BBCAfricaEye #kenya