‘Tunaendesha maisha yetu tukitegemea Uchumi wa buluu’

  • | BBC Swahili
    376 views
    Idadi kubwa ya watu wanaoishi katika maeneo ya pwani huchangia kwa kiasi kikubwa katika uchumi wa dunia, mchango wao ukiwa na thamani ya takriban dola trilioni 1.5 za Kimarekani kwa mwaka, hii ni kwa mujibu wa Umoja wa mataifa. Katika pwani ya Kenya, baadhi ya vijana wanatumia rasilimali ya bahari ili kujikwamua kiuchumi kupitia shughuli mbalimbali, ikiwemo kuvutia watalii kupitia michezo ya baharini. Mwandishi wa BBC @frankmavura ametuandalia taarifa ifuatayo kutoka Mombasa, nchini Kenya. #tanzania #kenya #uchumiwabluu