Wafanyibiashara mjini Busia wakabiliana na askari wa kaunti hiyo

  • | West TV
    126 views
    Kizaazaa kimeshuhudiwa jumatatu mchana katikati ya mji wa Busia kati ya askari wa kaunti ya Busia na wafanyabiashara wa Soko Posta mjini humo, baada ya askari hao kuwataka wafanyabiashara waliokuwa wakiuza bidhaa zao kando kando ya barabara kuu kuondoka,ila wafanyibiashara wakadinda. Inahofiwa watu kadhaa huenda wamejeruhiwa katika purukushani hiyo ambapo askari wa kaunti walilazimika kutorokea kusalama wao walipoanza kushambuliwa kwa mawe na wafanyabiashara hao wenye ghadhabu