Mtengeneza kahawa wa kwanza mwanamke Rwanda

  • | BBC Swahili
    252 views
    Perpetue Mukamusinga anajulikana kama "Queen P" ni mtengeneza kahawa wa wa kwanza wa kike (barista) nchini Rwanda. Ndani ya miaka 15 ya kazi yake, amewafundisha zaidi ya wanawake 2000 kote ulimwenguni kutengeneza kinywaji cha kahawa na baadhi yao wameanzisha biashara zao. Mbali na uuzaji wa kahawa nje ya nchi, imekuwa maarufu zaidi nchini humo ambapo unywaji wake unashamiri huku kukiwa na maduka mengi kila kona. Mukamusinga alichukua jukumu kubwa katika kuunganisha wakulima wa kahawa katika maeneo ya vijijini na soko la kimataifa. Mwandishi wa BBC Yves Bucyana alikutana naye na kuandaa taarifa hii #bbcswahili #rwanda #kahawa Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw