Ndani ya kundi la chuki dhidi ya wageni Afrika Kusini

  • | BBC Swahili
    1,464 views
    BBC Africa Eye imechunguza kuongezeka kwa chuki dhidi ya wageni nchini Afrika Kusini na ghasia zinazowalenga wahamiaji. Mtandao wa makundi unaopinga wahamiaji umeibuka nchini Afrika Kusini ukiwalaumu wahamiaji haramu kwa hali ya uchumi wa nchi, ukosefu wa makazi na matumizi ya dawa za kulevya. Lakini wakosoaji wanawashutumu kwa kusababisha ghasia wakiwalenga watu wanaoishi mazingira magumu. BBC Africa Eye inapata nafasi adimu ya kufika katika operesheni Dudula, kikundi maarufu zaidi cha kupinga wahamiaji nchini Afrika Kusini, wanapoingia barabarani na kupigania mamlaka ya kisiasa. #bbcswahili #bbcafricaeye #afrika Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw