Umuhimu wa Kichuri kwa Wakurya Tanzania

  • | BBC Swahili
    885 views
    Kabila la wakurya mkoani mara hutumia asusa maalumu almaarufu ‘KICHURI’ inayotokana na mabaki ya chakula kwenye tumbo la ngo’mbe au mbuzi baada ya kuchinjwa. KIchuri hutumika na watu wa rika zote na jinsia zote hasa kula nyama choma ijapokua wenyeji wanasema unaweza pia kuchemsha na kunywa na supu au chakula chochote kingine Mwandishi wa BBC Eagan Salla alizungumza na Mzee Samweli Mangaraya ambaye alimueleza namna inavyotengezwa na ni kwanini ni kiungo muhimu kwenye milo ya wakurya. 🎥 @eagansalla_gifted_sounds #bbcswahili #tanzania #mila Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw