Hali ya kibinadamu ya Tigray ni 'mbaya' mwaka mmoja baada ya makubaliano ya amani

  • | BBC Swahili
    427 views
    Ni mwaka mmoja tangu makubaliano ya amani yakubaliwe kumaliza mzozo wa umwagaji damu katika eneo la Tigray nchini Ethiopia, ambao ulisababisha vifo vya maelfu ya watu. Ingawa amani imedumu, watu wengi wameshindwa kurejea nyumbani kwani sehemu za eneo hilo bado zinakaliwa na vikosi vya Eritrea upande wa kaskazini na wanamgambo wa Amhara upande wa magharibi. Wengi wamekimbia makazi yao na wanahitaji misaada ya kibinadamu. Tulienda Shire, kaskazini-magharibi mwa Tigray, ili kuzungumza na watu ambao bado wanapambana na athari ya vita. #bbcswahili #ethiopia #eritrea Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw