Idadi ya watu walioaga dunia kutokana na ajali za barabarani imepungua mwaka huu

  • | Citizen TV
    850 views

    Idadi ya watu walioaga dunia kutokana na ajali za barabarani mwezi huu imepungua kwa asilimia nane ikilinganishwa na muda sawia mwaka jana. Akitoa takwimu hizi hii leo, mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya usalama wa barabarani George Njau alibaini kuwa japo taifa lilinakili upungufu huo, idadi ya majeruhi iliongezeka maradufu. Aidha, shirika la Directline assurance lilitoa hamasisho kwa madereva kuzingatia kanuni za trafiki ili kuepuka maafa.