Kaunti ya Baringo huenda ikatambuliwa na shirika la UNESCO kuwa hifadhi ya vitu vya kale

  • | KBC Video
    29 views

    Kwa kufahamika kuwa na ziwa lenye chemchemi za maji moto na Flamingo, kaunti ya Baringo huenda hivi karibuni ikatambuliwa na shirika la umoja wa mataifa la saransi na elimu UNESCO kuwa hifadhi ya vitu vya kale. Hii inafuatia kutambuliwa hivi majuzi kwa vifaa vya mawe vinavyoaminika kutumika miaka elfu 350 iliyopita katika kingo za ziwa Bogoria na watafiti na wanasayansi wakati wa mradi wa uchimbaji wa vifaa avya kale.Kulingana na makavazi ya kitaifa, uvumbuzi huo umeiweka nchi hii kwenye ramani ya dunia ya maeneo yaliyo na vifaa vya kale, kuimarisha utalii na vile vile kulifungua eneo hilo kwa ufumbuzi zaidi.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #Kenya #News