Japan yakamilisha rekodi yake ya bajeti ya ulinzi ya Yen trilioni 7.7 kwa mwaka wa fedha wa 2024

  • | VOA Swahili
    74 views
    Japan siku ya Ijumaa ilikamilisha rekodi yake ya bajeti ya ulinzi ya yen trilioni 7.7 kwa mwaka wa fedha wa 2024, mwaka wa pili mfululizo ambapo nchi hiyo iliongeza matumizi yake ya ulinzi kwa karibu trilioni moja ya Yen kutoka mwaka uliopita. Bajeti iliyoidhinishwa inaiweka Japan katika mstari wa kuongeza matumizi ya kijeshi kwa yen trilioni 43 kwa muda wa miaka mitano kuimarisha ulinzi katika mazingira magumu ya usalama na China inayozidi kuwa na msimamo na Korea Kaskazini isiyotabirika.