'Kitu gani watu wasiokuwa na hatia wamefanya kustahili kuuwawa...?'

  • | VOA Swahili
    272 views
    Jeshi la Israeli lilisema vikosi vyake vimepiga zaidi ya “malengo 100” kote huko Gaza katika kipindi cha saa 24, ikiwemo sehemu za kijeshi, sehemu zinakorushwa roketi na ghala za silaha. Ndege ya kivita ilipiga eneo katikati ya Bureij usiku kucha, liliuwa “magaidi wenye silaha w katika maficho yao” baada ya kile jeshi ilichokielezea katika taarifa yake kuwa ni jaribio la kushambulia kifaru cha Israeli. “Idadi kadhaa” ya wanamgambo wa Palestina waliuawa katika mapambano huko Khan Yunis, mji mkubwa ulioko kusini mwa Gaza ambao umekuwa ndiyo sehemu muhimu ya mapigano, jeshi lilisema. Kulingana na pendekezo lililotolewa na Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant, vita vitaendelea hadi pale Israel itapovunja “uwezo wa kijeshi na utawala” wa Hamas na uwezo wao wa kutawala” na kuwakomboa waliotekwa Oktoba 7. Israel ilianzisha kampeni dhidi ya kundi Hamas kufuatia mashambulizi ya Oktoba 7 ambayo yaliuwa watu 1,140 nchini Israel wengi wao wakiwa ni raia, kulingana na idadi ya AFP iliyotumia takwimu rasmi za Israeli. Wanamgambo hao pia waliwateka watu 250, 132 wakiwa bado wanashikiliwa, kulingana na Israel, wakiwemo watu 24 wanaoaminika kuwa waliuawa. Mashambulizi ya mabomu yasiyosita na uvamizi wa ardhini unaofanywa na Israeli umeuwa watu wasiopungua 22,438 wengi wao wanawake na watoto, kulingana na wizara ya afya ya Gaza. - AFP #Haifa ⁣⁣⁣⁣ #Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #GalMeirEizenkot #GadiEizenkot #wazirimkuu #jerusalem #alaqsa #msikiti #ibada #ijumaa #gaza #mauaji #jeshi #israel #voa #voaswahili