- 284 viewsMtoto wake, Hamza Al-Dahdouh, aliuawa katika shambulizi la anga lililofanywa na Israeli akiwa kwenye gari karibu na Rafah pamoja na Mustafa Thuraya, kulingana na maafisa wa afya na umoja wa waandishi wa habari huko Gaza. Wapalestina wote wawili walikuwa waandishi wa habari wa kujitegemea. Wa tatu alikuwa mwandishi wa kujitegemea ambaye alijeruhiwa. Al- Dahdouh alikuwa akifanya kazi na Al Jazeera, ambako baba yake Wael Al-Dahdouh ni mwandishi kiongozi wa kituo hicho huko Gaza. Wael Al-Dahdouh alikuja kuwa mashuhuri kwa watazamaji kote Mashariki ya Kati baada ya kufahamu wakati wa matangazo mubashara kuwa mke wake, mtoto wake mwengine wa kiume, binti yake na mjukuu wake wa kiume walikuwa wameuawa katika shambulizi la anga lililofanywa na Israeli. Al-Dahdouh alisema: “Vipi mtu anaweza kupokea habari za kifo cha mtoto wake wa kwanza wa kiume na ndiyo kila kitu katika maisha yangu baada ya kuwapoteza baadhi ya wanafamilia wangu; mke wangu, mtoto wangu Mahmoud na Sham na Adam. Vipi naweza kuipokea habari hii?” Majeshi ya Ulinzi ya Israel hayakutoa majibu mara moja walipotakiwa kutoa maelezo. Imekuwa ikipiga mabomu katika eneo la Palestina tangu uvamizi wa Hamas wa mashambulizi ya kuvuka mpaka ya Oktoba 7 ambapo maafisa wa Israeli wanasema watu 1,200 waliuwawa. Siku ya Jumapili (Januari 7), wizara ya afya ya Gaza ilisema shambulizi la Israel limeuwa Wapalestina 22,835 hadi sasa. “Ulimwengu lazima uone kwa macho yao na siyo kwa macho ya Israel. Ni lazima isikilize na kuangalia kila kinachotokea kwa Wapalestina. Nini alichofanya Hamza kwao na nini ambacho familia yangu imewafanyia? Nini walichofanyiwa na raia wa Ukanda wa Gaza? Hawa wote hawajafanya kitu chochote," alisema Al-Dahdouh. Kamati ya Kuwalinda Waandishi wa Habari, chombo cha kimataifa kinachofuatilia waandishi, kilisema Jumamosi, waandishi 77 na wafanyakazi wa vyombo vya habari waliuwawa, kati yao Wapalestina 70, Waisraeli wanne na Walebanon watatu. - Reuters #Haifa #waelaldahdouh #hamzaaldahdouh #Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #GalMeirEizenkot #GadiEizenkot #wazirimkuu #jerusalem #alaqsa #msikiti #ibada #ijumaa #gaza #mauaji #jeshi #israel #voa #voaswahili #mwandishi #aljazeera
Mwandishi Kiongozi wa Al Jazeera: 'Ulimwengu lazima uone kwa macho yao...'
- - Suagar Boy ››
- 30 Nov 2024 - The finance chief of India's Adani Group on Friday rejected U.S. allegations that executives, including Chairman Gautam Adani, were part of a Ksh.34 billion bribery scheme, while the Indian government said it has not received any U.S. request on the…
- 30 Nov 2024 - Disaster response teams coordinated by National Government Administration have begun evacuating over 240 households affected by the ongoing floods.
- 30 Nov 2024 - European and American carmakers are set to lose up to 17 per cent of their combined annual core profits if the U.S. imposes import tariffs on Europe, Mexico and Canada, S&P Global said in a report on Friday, warning of potential credit downgrades.
- 30 Nov 2024 - The Sambaza Furaha na Safaricom caravan was on Friday in its fifth day this week traversing the areas of Homa Bay, Rodi Kopany, Rongo, and Awendo.
- - Shame of Nakuru's dead not resting in peace: County fights claims of reuse of graves
- 29 Nov 2024 - Almost two months have lapsed since the Universal Health Coverage, through the Social Health Authority (SHA), was rolled out and the enrolment numbers into the programme are not yet up to the expected levels, with only 16 million registrations to date.
- 29 Nov 2024 - DCI officers spent the better part of Friday questioning some of the leaders and members of the public who attended the chaotic burial ceremony in Limuru, which saw goons attack former Deputy President Rigathi Gachagua and mourners.
- 29 Nov 2024 - The Jaramogi Oginga Odinga University of Science and Technology (JOOUST) will conduct an audit on all 2024 graduates before awarding any certificate amid reports of irregular awarding of degrees at the institution.
- 29 Nov 2024 - The Kenya Union of Clinical Officers (KUCO) has threatened to down their tolls beginning December 23, 2024 over what they term as discrimination in the rollout of the Social Health Insurance Fund (SHIF).
- 29 Nov 2024 - The Kenya Union of Clinical Officers (KUCO) has threatened to down their tolls beginning December 23, 2024 over what they term as discrimination in the rollout of the Social Health Insurance Fund (SHIF).