Mtoto wa Kipalestina miaka nane aeleza madhila yanayo wakabili

  • | VOA Swahili
    550 views
    Tangu kuanza kwa vita huko Gaza, Abdel Jaber Mohammed al-Farra alisema amepoteza vitu vingi – makazi yake, ujirani wake na shule yake. Farra na familia yake walikimbia makazi yao katikaujirani wa al-Manara upande wa mashariki ya Khan Younis baada ya majeshi ya Israeli kupiga bomu jengo. “Eneo tunaloishi liko salama, lina msikiti, ambako jina la Mungu linatukuzwa. Hakuna kitu, sote ni watu wa amani, hakuna kitu kibaya chochote katika ujirani wa al-Manara, ni salama na kimya, na eneo liko wazi,” alisema baba wa Abdel Jaber, Mohammed. Baada ya kushindwa kupata sehemu katika shule ambayo tayari imefurika watu waliokoseshwa makazi katika eneo, familia hiyo imekuwa ikiishi usiku kucha kila siku nje ya shule kwenye vibaraza. “Tuliweka vichwa vyetu chini na kujifunika na taulo, hadi asubuhi ilipoingia,” alisema Abdel Jaber. “Hali ni ya msiba mkubwa. Tunayaomba mataifa yote kututumia misaada, kufungua kivuko cha mpakani cha Rafah, ili kuleta misaada, na kumaliza vita. Malizeni hii dhulma dhidi yetu. Nyumba zetu zote zimepigwa mabomu,” alisema mtoto huyo wa miaka nane. Majeshi ya Ulinzi ya Israel yamekuwa yakipiga mabomu katika eneo la Palestina tangu uvamizi wa Hamas wa mashambulizi ya kuvuka mpaka ya Oktoba 7 ambapo maafisa wa Israeli wanasema watu 1,200 waliuwawa.⁣ Mashambulizi ya Israeli yameua zaidi ya Wapalestina 23,000, kuharibu sehemu kubwa ya Gaza na kuwakosesha makazi wengi angalau kati ya watu milioni 2.3, ikileta hali ya taharuki na mgogoro mbaya sana wa kibinadamu. - Reuters #Haifa ⁣⁣⁣⁣⁣#waelaldahdouh #hamzaaldahdouh⁣⁣ #Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #GalMeirEizenkot #mauaji #jeshi #israel #voa #voaswahili #mwandishi #aljazeera