Wafanyakazi wa Shirika la Mwezi Mwekundu la Palestina wakiipakia miili

  • | VOA Swahili
    359 views
    Shirika la Mwezi Mwekundu la Palestina Jumanne (Januari 9) liliiondoa miili miwili baada ya raia kushambuliwa kwa mabomu katika kambi ya wakimbizi ya Maghazi katikati mwa Gaza, lilieleza katika mtandao wa kijamii wa X. Shirika hilo la kibinadamu lilitoa picha za video za wafanyakazi wake wakipakia miili miwili iliyokuwa katika sanda ndani ya gari la wagonjwa. Shirika la habari la Reuters lilithibitisha tarehe na eneo ilipochukuliwa video hiyo na lilithibitishiwa na mwakilishi wa Mwezi Mwekundu Nebal Fersakh. Jeshi la Isreali Jumatatu (Januari 8) lilisema limepiga mabomu eneo lililokuwa na silaha katikati ya Maghazi, na Jumanne lilisema ndege yake iliwashambulia wapiganaji wa Hamas katikati ya Gaza ilipo kambi ya wakimbizi. Eneo la kusini na kati mwa Gaza limekuwa ndiyo linalolengwa na mashambulizi ya Israel, ambapo siku ya Jumamosi (Januari 6) ilitangaza miundombinu ya Hamas upande wa kaskazini imebomolewa. Majeshi ya Ulinzi la Israel yamekuwa yakipiga mabomu katika eneo la Palestina tangu uvamizi wa Hamas wa mashambulizi ya kuvuka mpaka ya Oktoba 7 ambapo maafisa wa Israeli wanasema watu 1,200 waliuwawa.⁣⁣ ⁣ Mashambulizi ya Israeli yameua zaidi ya Wapalestina 23,000, kuharibu sehemu kubwa ya Gaza na kuwakosesha makazi wengi angalau kati ya watu milioni 2.3, ikileta hali ya taharuki na mgogoro mbaya sana wa kibinadamu. - Reuters⁣ #Haifa ⁣⁣⁣⁣⁣#waelaldahdouh #hamzaaldahdouh #shirikalamwezimwekundu #Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #GalMeirEizenkot #mauaji #jeshi #israel #voa #voaswahili #mwandishi #aljazeera #maghazi