Israeli: Maelfu ya watu wakusanyika kufanya maombi ya kuachiliwa kwa mateka

  • | VOA Swahili
    463 views
    Maelfu ya watu walikusanyika kufanya maombi ya kuachiliwa kwa mateka waliosalia wanaoendelea kushikiliwa Ukanda wa Gaza Jumatano mahali ulipo ukuta wa Western Wall Jerusalem. Eneo ambapo maombi yalifanyika Jumatano na umati wa watu ni sehemu takatifu sana kwa Wayahudi kufanya maombi. Hatma ya mateka hao inawatia wasiwasi Waisraeli na kuachiliwa kwao bado ni moja ya malengo ya serikali ya Israel katika vita yake dhidi ya Hamas. Katika shambulizi lao la Oktoba 7, Hamas na wanamgambo wengine waliwateka takriban watu 250, wakiwemo wanaume, wanawake na watoto na wazee. Kiasi cha watu 110 wameachiliwa na wengine 110 wanashikiliwa, na huku watu 20 hivi ambao waliuawa wakiwa wanashikiliwa, mamlaka za Israeli zinasema. Mateka walioachiliwa wametoa maelezo ya kuhuzunisha walioshuhudia wakati wakishikiliwa, ambapo wengine walipewa chakula kidogo, kulazwa sakafuni na kuhofia maisha yao wakati wote huo. Shambulizi lililofanywa na Hamas Oktoba 7 kwa kuvuka Gaza na kuingia kusini mwa Israel lilisababisha vita na waliwauwa kiasi cha watu 1,200. Mashambulizi ya Israel ya angani, ardhini na baharini huko Gaza yameuwa zaidi ya Watu 23,000, theluthi mbili kati ya hao ni wanawake na watoto, kulingana na Wizara ya Afya katika eneo la Gaza linalosimamiwa na Hamas.⁣ Idadi hiyo haitofautishi kati ya raia na wanamgambo. - AP #Haifa ⁣⁣⁣⁣⁣#waelaldahdouh #hamzaaldahdouh #shirikalamwezimwekundu⁣⁣ #Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #GalMeirEizenkot #mauaji #jeshi #israel #voa #voaswahili #mwandishi #aljazeera #maghazi #westernwall #mateka #jeshi