Mji wa Rafah umegeuka kuwa kambi ya Wapalestina waliokimbia makazi yao

  • | VOA Swahili
    391 views
    Kambi mbalimbali za muda zinazo wahifadhi Wapalestina waliokoseshwa makazi zimefunguliwa huko Rafah karibu na mpaka wa Misri, eneo la kusini mwa Ukanda wa Gaza, huku vita ikiendelea kati ya Israel na kikundi cha wanamgambo wa Kipalestina, Hamas. Wakazi wa Gaza walijificha Jumatatu kuepuka mashambulizi ya nguvu ya mabomu na bunduki katika mji wa Khan Yunis, huku shinikizo likiongezeka kwa Israel kuwa hatimaye kuwe na suluhisho la mataifa mawili jambo ambalo limekuwa ni matakwa ya Wapalestina. Walioshuhudia wameripoti mashambulizi hatari na mapigano makali kati ya wanajeshi wa Israeli na wanamgambo wa Hamas yaliyoendelea usiku kucha kusini mwa mji huo ambao ni chimbuko la vita vya hivi karibuni. Wizara ya afya katika eneo linalodhibitiwa na Hamas iliripoti Jumatatu kuwa zaidi ya watu 120 waliuawa katika kipindi cha saa 24. Shambulizi lililofanywa na Hamas Oktoba 7 kwa kuvuka Gaza na kuingia kusini mwa Israel lilisababisha vita na waliwauwa kiasi cha watu 1,200.⁣⁣ ⁣ Mashambulizi ya Israel ya angani, ardhini na baharini huko Gaza yameuwa zaidi ya Watu 25,295, wengi wao ni wanawake na watoto, kulingana na Wizara ya Afya katika eneo la Gaza linalosimamiwa na Hamas.⁣ Idadi hiyo haitofautishi kati ya raia na wanamgambo. - AP⁣ #Haifa ⁣⁣⁣⁣⁣#waelaldahdouh #hamzaaldahdouh #shirikalamwezimwekundu⁣ #Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #GalMeirEizenkot #mauaji #jeshi #israel #voa #voaswahili #mwandishi #aljazeera #maghazi #khanyounis