Maandamano ya Chadema yafanyika, wananchi wajitokeza

  • | VOA Swahili
    1,844 views
    Idadi kubwa ya Watanzania wamejitokeza na kuunga mkono maandamano ya amani yaliyoandaliwa na chama kikuu cha upinzani Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) yaliyofanyika Jumatano. Maandamano hayo yaliyoanzia jijini Dar-es Salaam, na kuendelea katika miji mingine yanapinga kupanda kwa gharama za maisha na kudai kusikilizwa kwa maoni ya wananchi na wadau wa demokrasia katika masuala ya sheria ya uchaguzi. Waongozi wa maandamano hayo walifikisha ujumbe wao katika ofisi za Umoja wa Mataifa, unaoitaka serikali ya Tanzania kushughulikia changamoto za kupanda kwa gharama za maisha zinazowakabili wananchi pamoja na mageuzi ya katiba. Mratibu wa mtandao wa vuguvugu la katiba, Buberwa Kaiza amesema sababu ya maandamano hayo kuishia katika ofisi za Umoja wa Mataifa ni kutoa ujumbe duniani kupitia umoja huo kuwa miswaada ya sheria ya uchaguzi iondolewe bungeni. “Sababu kubwa ya kuja hapa Umoja wa Mataifa ni kutoa ujumbe duniani kote kupitia umoja huu kwamba madai haya ya sheria hizi ziondolewe bungeni yapate nguvu yaweze kusikilizwa kwa namna ambavyo inatarajiwa,” Kaiza. #chadema #upinzani #maandamano #wananchi #daressalaam #tanzania #voa #voaswahili