Droni za Russia zashambulia Odesa zikiharibu kiwanda na miundombinu

  • | VOA Swahili
    800 views
    Ndege zisizo kuwa na rubani zimeshambulia kwa mabomu Odesa usiku wa Jumatano (Januari 24), zikiharibu majengo ya makazi ya watu, jengo la kiwanda na miundombinu ya uraiani, kulingana na taarifa za maafisa. Gavana wa mkoa wa Odesa Oleh Kiper alisema kupitia mtandao wa Telegram kuwa watu wanne walijeruhiwa wakati wa shambulizi hilo katika mji wa bandari ulioko Black Sea. Russia ilirusha droni 14 na makombora matano kushambulia Ukraine usiku kucha, jeshi la anga la Ukraine lilisema Alhamisi (Januari 25), kuwa mifumo ya ulinzi wa anga ilitungua droni 11. Jeshi la anga lilisema kupitia ujumbe wake wa Telegram kuwa Russia ililenga zaidi kusini mwa Ukraine. - Reuters #rais #vladimirputin #uhaini #wagner #usaliti #russia #joebiden #marekani #wagnergroup