Wakulima wenye hasira wawasha moto kupinga mpango wa serikali kupunguza ruzuku

  • | VOA Swahili
    479 views
    Wakulima wenye hasira walichoma matairi na uchafu Ijumaa (Januari 26) pembeni ya barabara kuu ya A20, wakipinga mpango wa serikali kupunguza pole pole ruzuku ya diesel inayotumika katika kilimo. Kanda ya video ya aliyeshuhudia tukio hilo pia ilionyesha uchafu ukitupwa nje ya ofisi ya serikali katika mji wa Montauban. Serikali ya Ufaransa baadae ilitangaza itasitisha mipango ya kuondoa ruzuku kwa ajili ya mafuta ya diesel lakini hilo halijatosha kuwaridhisha wakulima ambao wametishia kukusanyika katika mji mkuu Paris na matrekta yao. Wakulima wa Ufaransa wanaishutumu serikali kwa kutochukua hatua za kutosha kuwasaidia, ushindani usiolingana kati ya nchi jirani, na viwango vya kilimo kandamizi ambavyo ni gharama kubwa kuvifuata. Siku ya Ijumaa, kiongozi wa jumuiya kubwa kabisa ya wakulima Ufaransa –the FNSEA- alisema anatoa wito kwa wanachama wote kuendelea na harakati za kupinga mpango wa kupunguzwa ruzuku, hata baada ya serikali kusema ilikuwa na mpango wa kuboresha hali ya maisha na mazingira ya kazi ya wakulima. - Reuters. #wakulima #Ufaransa #diesel #ruzuku #serikali #thibaultizoret #paris #montauban #voa #voaswahili