Hamas watoa kanda ya video walioihariri ikidai kumekuwa na mapigano mitaani

  • | VOA Swahili
    395 views
    Kitengo cha kijeshi cha kikundi cha wanamgambo wa Palestina Hamas kimetoa Jumatatu (Januari 29) video iliyohaririwa inayoonyesha mapigano katika mitaa ya Khan Younis huko Gaza. Kanda hiyo inawaonyesha wapiganaji wakiwa wamebeba mifumo ya kubebea silaha begani na kufyatua dhidi ya vifaru vya kivita. Reuters haikuweza yenyewe kuthibitisha eneo au tarehe ambayo video hiyo ilichukuliwa. Mapema Jumatatu, jeshi la Israeli lilisema wanajeshi wake waliwaua darzeni ya Wapalestina wenye silaha kote Ukanda wa Gaza ndani ya saa 24 zilizopita, wakiwemo wanne waliokuwa wameonekana wakijiandaa kuwashambulia wanajeshi waliokuwa karibu na hospitali ya Al- Amal huko kusini mwa Khan Younis. Kitengo cha kijeshi cha Hamas na kikundi cha Islamic Jihad vilisema wapiganaji wake walipambana na wanajeshi wa Israeli katika maeneo kadhaa katika eneo finyu usiku kucha. Kitengo cha kijeshi cha Hamas kilisema wapiganaji wake wameangamiza vifaru viwili vya Israeli huko Khan Younis. Shambulizi lililofanywa na Hamas Oktoba 7 kwa kuvuka Gaza na kuingia kusini mwa Israel lilisababisha vita na waliwauwa kiasi cha watu 1,200.⁣⁣ Maafisa wa afya wa Palestina walisema watu wasiopungua 26,000 wakazi wa Gaza wameuawa katika vita hivyo. - Reuters⁣⁣ ⁣ ⁣⁣⁣#Haifa ⁣⁣⁣⁣⁣#waelaldahdouh #hamzaaldahdouh #shirikalamwezimwekundu⁣⁣⁣⁣⁣⁣ ⁣⁣⁣⁣⁣ #Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #GalMeirEizenkot #mauaji #jeshi #israel #voa #voaswahili #mwandishi #aljazeera #maghazi #khanyounis