Daktari: 'Yalikuwa mashambulizi makubwa ya mabomu, hatukulala usiku kucha'

  • | VOA Swahili
    393 views
    Daktari mmoja katika Hospitali ya Khan Younis Nasser alisema kuwa jeshi la Israeli lilikuwa linawaamrisha Wapalestina kuondoka katika eneo kwa kuonyesha ujumbe kutoka katika quadcopter katika video iiyotolewa Jumatatu (Januari 29). Daktari Ahmed Moghrabi aliipiga picha quadcopter iliyokuwa inazunguka karibu na hospitali hiyo na pia mawingu ya moshi mweusi yaliyokuwa angani, akisema hakuweza kulala kutokana na mashambulizi makali ya mabomu usiku kucha. Reuters iliweza kuthibitisha eneo la tukio kuwa ni hospitali ya Nasser huko Khan Younis, Gaza kutokana na majengo na ukuta unaonekana katika video ambayo inalingana na picha za satellite za eneo hilo. Reuters haikuweza kuthibitisha peke yake lini video hii ilichukuliwa. Mashambulizi ya anga yalipiga mji wa kusini wa Khan Younis siku ya Jumatatu. Israel ilisema kuwa watu kati ya darzeni ya Wapalestina waliokuwa na silaha waliwaua katika muda wa saa 24 zilizopita ambapo walikuwa wanajiandaa kushambulia wanajeshi waliokuwa karibu na hospitali ya Al-Amal iliyoko takriban kilomita 1 (maili 0.6) kutoka Hospitali ya Nasser. Majengo ya hospitali yalikuwa hatarini kuanguka huko Khan Younis , wizara ya afya ya Gaza imetahadharisha Jumapili (Januari 28). Shambulizi lililofanywa na Hamas Oktoba 7 kwa kuvuka Gaza na kuingia kusini mwa Israel lilisababisha vita na waliwauwa kiasi cha watu 1,200.⁣⁣⁣ Maafisa wa afya wa Palestina walisema watu wasiopungua 26,000 wakazi wa Gaza wameuawa katika vita hivyo. - Reuters⁣⁣⁣ ⁣ ⁣⁣ ⁣⁣⁣#Haifa ⁣⁣⁣⁣⁣#waelaldahdouh #hamzaaldahdouh #shirikalamwezimwekundu⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣ ⁣⁣⁣⁣⁣⁣ #Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #GalMeirEizenkot #mauaji #jeshi #israel #voa #voaswahili #mwandishi #aljazeera #maghazi #khanyounis