Mashabiki wa Ivory Coast wakishangilia kuondoshwa Senegal

  • | VOA Swahili
    212 views
    Frank Kessie amefunga bao la penalty la ushindi kwa taifa ambalo ni wenyeji wa michezo ya AFCON, Ivory Coast wakimchapa bingwa mtetezi Senegal 5-4 na kujipatia tiketi ya kuingia robo fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika. Ilikuwa ni kiki ya pili iliyofuzu ya Kessie katika mechi hiyo baada kuingia uwanjani kama mchezaji mbadala na kusababisha sare 1-1 katika muda wa kawaida pamoja na penalty ya dakika 86 huko Yamoussoukro. Beki wa Senegal Moussa Niakhate alikosa penalty ya tatu katika kupiga mpira. Ryan Mendes alifunga penalty ya dakika ya mwisho kwa Cape Verde kufikia robo fainali kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mauritania. - AP #AFCON #IvoryCoast #Senegal #football #soccer #voaswahili