Chile: Maelfu ya nyumba zaangamia, mioto zaidi ya 90 inaendelea kuwaka

  • | VOA Swahili
    393 views
    Mioto ya misituni inayoenea kote katikati mwa Chile imeuwa idadi kubwa ya watu na mamia hawajulikani walipo katika kile kilichokuwa ni janga baya sana la kitaifa nchini humo ambalo halijatokea kwa zaidi ya muongo mmoja. Mioto hiyo ya misituni ilianza siku kadhaa zilizopita inatishia usalama katika maeneo ya mpaka wa Vina del Mar na Valparaiso. Miji miwili ya pwani ambayo ni maarufu kwa watalii na ikichanganywa na wakazi zaidi ya milioni moja. Kanda ya video iliyochukuliwa kwa Droni na Reuters huko eneo la Vina del Mar ilionyesha eneo lote jirani limeungua. Pedro Quezada alikabiliwa na moto na kuipoteza nyumba yake. “Upepo ulikuwa mbaya, na joto lilikuwa linaunguza. Hapakuwa na kupumua. Watu walitawanyika kila mahali.” Mamlaka nchini Chile wameanzisha amri ya kutotoka nje kuanzia saa tatu usiku katika eneo lililoathiriwa vibaya sana na kupeleka majeshi kuwasaidia zima moto kuzuia kuenea kwa mioto hiyo. Maafisa wanasema kiasi cha maelfu ya nyumba zimeangamia, huku mioto zaidi ya 90 ikiendelea kuwaka kute Chile. Sergio na Maria walirejea katika kile kilichokuwa kimesalia kwenye nyumba yao Jumapili kuokoa kile walichoweza kukipata. Pamoja na vitu venye thamani vya familia, Karakana ya Sergio ilikuwa pia imeungua. Familia hiyo, hivi sasa wakiwa na miaka 60, wana wasiwasi kwamba itawalazimu kuanza maisha upya. “Mikono yetu imefungika. Hii ni karakana yangu, tunaishi hapa. Yote tuliyofanya na kukusanya , katika maisha yetu yote.” Rais Gabriel Boric Jumapili alitangaza siku mbili za maombolezo ya kitaifa na kusema nchi ijiandae kwa habari mbaya zaidi. Pia alitoa taarifa ya hali ya hivi sasa katika juhudi za kupambana na mioto. “Tumesema hilo, na tunarejea kusema – leo kipaumbele ni kuokoa maisha kwani bado kuna mioto inayoendelea kuwaka; kuwasaidia majeruhi, na kuidhibiti mioto inayowaka ambayo inaendelea kuzimwa.” Licha ya kuwa mioto ya misituni siyo ya kawaida wakati wa kipindi cha joto Chile, mlolongo wa mioto hii ya karibuni imekuwa yenye uangamivu zaidi kuliko kawaida – janga baya zaidi tangu tetemeko la mwaka 2010 kutokea ambapo watu takriban 500 walifariki. #mioto #chile #misitu #maangamizi #nyumba #zimamoto #curfew #polisi #voa #voaswahili