Waandamanaji, mapambano katika mitaa ya Dakar baada ya uchaguzi wa rais kuahirishwa

  • | VOA Swahili
    101 views
    Wabunge wa Senegal Jumatatu walijadili hali iliyokuwa haijawahi kutokea ya hatua ya kuahirisha uchaguzi wa rais uliokuwa ufanyike mwezi huu, ambao ulisababisha mapambano ghasia nje ya bunge na kuleta wasiwasi kimataifa. Vikosi vya usalama vilitumia mabomu ya machozi kuvitawanya vikundi vidogo vya waandamanaji wa upande wa upinzani nje ya Bunge la Taifa. Waandamanaji walikuwa wakiimba “Macky Sall ni dikteta” wakikusudia rais wa nchi hiyo baada ya kutawanywa. Mapambano ya mara kwa mara yalikuwa nadra kuonekana katika eneo ambalo kwa kawaida ni tulivu mjini Dakar, ambako polisi na vikosi vya usalama vikisaidiwa na magari makubwa yalipelekwa kulilinda bunge. - AFP #senegal #mackysall #voaswahili