Vyanzo vya ulinzi: Uharibifu ulioletwa na shambulizi la Israeli

  • | VOA Swahili
    273 views
    Watu walikusanyika Alhamisi asubuhi (Februari 15) mji wa Nabatieh ulioko kusini mwa Lebanon karibu na magari ya kubeba wagonjwa, wakikagua uharibifu na kifusi cha jengo lililopigwa kwa kile vyanzo vilisema ilikuwa ni shambulizi la Israeli. Shambulizi hilo katika jengo Jumatano jioni (Februari 14) liliuwa wanawake wasiopungua watatu, watoto kadhaa na mwanaume mmoja, kulingana na mkurugenzi wa hospitali ya mji huo, Hassan Wazni, na vyanzo vingine vitatu vya usalama. Watu kadhaa pia walijeruhiwa, Wazni aliliambia shirika la Reuters. Mwanamke mmoja na watoto wawili waliuawa katika shambulizi jingine mapema siku hiyo. Wanamgambo wa Hezbollah kadhaa waliuawa pia na shambulizi hilo la Israeli katika vijiji vilivyopo kusini mwa Lebanon siku ya Jumatano, vyanzo vitatu vya usalama vya Lebanon vilisema, wakati Israel ilisema ilijibu shambulizi la roketi la Hezbollah ambalo lilimuua mwanajeshi wake. Hezbollah na jeshi la Israeli wamekuwa wakishambuliana kwa silaha katika mpaka wa Israel na Lebanon kwa zaidi ya miezi minne, baada ya kikundi chenye silaha cha Lebanon kushambulia kwa roketi upande wa pili wa mpaka ambao unagombaniwa wakiwaunga mkono washirika wake Wakipalestina Hamas. #Haifa ⁣⁣⁣⁣⁣#waelaldahdouh #hamzaaldahdouh #shirikalamwezimwekundu⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣ #Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #GalMeirEizenkot #mauaji #jeshi #israel #voa #voaswahili #mwandishi #aljazeera #maghazi #wahouthi #marekani #uingereza #shambulizi #dhamar #yemen #iran