Idadi ya watu waliouwawa Nkararo yafikia watu wanne

  • | Citizen TV
    566 views

    Hali ya taharuki bado imetanda katika eneo la Transmara kaunti ya Narok baada ya mtu mmoja zaidi kuuwawa mapema leo. Idadi ya waliofariki kufikia sasa ni watu wanne baada ya shamba la miwa kuteketezwa katika mpaka wa Nkararo-Enoreteet. OCPD wa eneo la Transmara West Jamleck Ngaruiya, amesema maafisa wa usalama kutoka vitengo tofauti wanaendelea kuwasaka wahusika katika eneo hilo la mpaka.