Ukosefu wa usalama Bahari ya Shamu kuathiri usambazaji wa chakula Ramadhani

  • | BBC Swahili
    457 views
    Ukosefu wa usalama katika Bahari ya Shamu kutokana na mashambulizi ya makundi ya Houthi kwa meli umetatiza uwasilishaji wa bidhaa kwa maeneo ya Afrika Mashariki, hali ambayo inatishia kuongeza gharama ya Maisha katika eneo hili. Hali hii imeleta ongezeko la bei za bidhaa, ikiwemo vyakula muhimu katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa Waislamu kama vile tende Peter Mwangangi ametembelea mji wa Mombasa katika pwani ya Kenya, ambapo anaangazia hali ilivyo miezi miwili baada ya mashambulio ya Houthi kuanza. #bbcswahili #kenya #mwezimtukufu Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw