Hali ya kisiasa Haiti yaendelea kuwa tete

  • | VOA Swahili
    171 views
    Hali ya kisiasa nchini Haiti bado ni tete siku moja baada ya waziri mkuu Ariel Henry, kusema kwamba anajiuzulu baada ya kuundwa baraza la mpito la uongozi, ingawa wakuu wa magenge ya uhalifu wanasisitiza kuhusishwa kwenye mipango yeyote ya kuunda serikali ya mpito. Henri alikubali kujiuzulu Jumatatu wakati wa mkutano wa dharura wa Jumuia ya mataifa ya Caribean CARICOM, nchini Jamaica, ambako waziri wa mambo ya nje wa Marekani aliahidi msaada wa ziada wa zaidi ya dola milioni 100 kuwezesha kupelekwa kikosi cha kimataifa nchini humo. #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.