'Jimbo letu liko katika mshtuko'
Kikosi cha uokoaji na utafutaji kina endelea na zoezi la kuwatafuta watu 20 waliotoweka baada ya daraja kuu kubomoka katika mji wa Baltimore, Maryland ulioko kusini mwa Marekani
Video iliyochukuliwa kwa simu ya mkononi ilionyesha vipande kadhaa vya Daraja la Scott Key likiporomoka ndani ya maji ya Mto Patapsco baada ya meli iliyobeba mizigo yenye bendera ya Singapore inayoitwa Dali kugonga nguzo inayoshikilia daraja majira ya saa kumi na moja alfajiri (05:30 UTC) Jumanne.
Mamlaka zinasema magari kadhaa yalikuwa juu ya daraja wakati ajali hiyo ilipotokea.
Maafisa wa huduma za dharura wa Baltimore kikosi cha watafutaji na waokoaji kinaendelea kuwatafuta watu wasiopungua 20 ambao wanasadikiwa kuwa ndani ya maji.
Magari kadhaa yalianguka kwenye maji baridi na waokoaji walikuwa wakitafuta zaidi ya watu saba.
Wanasema vyombo vyao vimebaini kuna magari yaliyotumbukia mtoni.
Inaonekana Meli hiyo iligonga nguzo moja ya daraja Fransis scott key Bridge ambapo lilivunjika vipande, kulingana na picha zilibandikwa katika mtandao wa X.
Meli hiyo ilisababisha moto ulitoa moshi mweusi ulopaa hewani.
Meli hiyo inayosafiri na bendera ya Singapore na jina la Dali ilikuwa imeondoka bandarini dakika 25 zilizopita ikielekea Singapore.
Synergy Marine Corp, Wasimamizi wa meli ya Dali, wametoa taarifa wakisema meli hiyo iligonga moja ya nguzo za daraja hilo na kuwa mabaharia wake wote, wakiwemo nahodha wa meli hiyo wamesalimika na hakuna ripoti zozote za majeruhi.
Daraja hilo lenye urefu wa kilomita 2.5 lenye umri wa miaka 47 ni kiungo kikuu katika njia kuu zinazounganisha majimbo zinazo zunguka mji wa Baltimore, moja ya bandari kadhaa kubwa kabisa za Marekani.
Ilipewa jina la Francis Scott Key, mwandishi wa “The Star Spangled Banner,” shairi ambalo baadae lilitengenezwa kuwa muziki na hatimaye kuwa ni nyimbo ya taifa ya Marekani.
Key alihamasishwa kuandika shairi baada ya kushuhudia mashambulizi ya bomu yaliyofanywa na Uingereza katika ngome kuu ya jeshi la Marekani huko Baltimore mwaka 1814. - VOA NEWS, AP, Reuters
#Daraja #baltimore #kubomoka #magari #mtoni #francisscottkeybridge #marekani
28 Nov 2024
- Kenya had a dismal November in the qualifiers.
28 Nov 2024
- The sentiment by the PS has necessitated an explanation on the citizenship of Kenyans.
28 Nov 2024
- The development comes hardly a week after students completed their KCSE exams.
29 Nov 2024
- Angry residents of Syokimau/Mlolongo Ward on Thursday forced their MCA to wade through muddy roads in a bid to show the deplorable state of the estate.
29 Nov 2024
- Leaders allied to former DP Rigathi Gachagua on Thursday evening visited the DCI headquarters on Kiambu Road in a bid to demand for quick probe into chaos that were witnessed earlier in the day during a burial in Limuru.
29 Nov 2024
- Former Standard Group employees are demanding payment of their salary arrears and SACCO savings, accusing the media house of failing to honor their redundancy and severance pay commitment after laying them off.
29 Nov 2024
- He claims his grandfather bought the land at Sh900 in 1947, now worth Sh3 billion.Mosques, churches, schools and government installations occupy the land.
29 Nov 2024
- ODM dismisses reports of coercion to vote by consensus
29 Nov 2024
- Private entities allowed to recover proceeds of graft
29 Nov 2024
- IEBC boss warns of constitutional crisis over boundaries review deadline
29 Nov 2024
- Kenya's high octane politics three years to next general elections
29 Nov 2024
- Savannah Clinker Chairman Benson Ndeta will spend the night in police custody after he was arrested on allegations of forgery, conspiracy to defraud, and uttering false documents.
29 Nov 2024
- Kenya ranked top in Africa in cyber-dependent crimes, ahead of Nigeria and South Africa. Index found Kenya ranked high in criminality, criminal markets and cybercrime actors.