Kampeni za uchaguzi Marekani zapambana kupata wapiga kura weusi

  • | VOA Swahili
    220 views
    Joe Biden na Donald Trump wameshinda uchaguzi wa awali katika vyama vyao kwenye jimbo la Magharibi kati la Wisconsin wiki hii, huku wote wakiwa na uhakika wa uteuzi. Wagombea hao wanapambana kwa ajili ya kushinda uchaguzi mkuu huko Wisconsin, ni moja ya majimbo yanayoweza kuamua ushindani wa mwaka 2024. Mwandishi wa VOA Scott Stearns anaripoti kuwa kampeni zinafanya kazi kupata uungaji mkono wa wapiga kura weusi huko Wisconsin. Wapiga kura wa Wisconsin walimchagua Donald Trump mwaka 2016 lakini Joe Biden miaka minne baadaye. Na mara zote ushindani ulikuwa wa karibu. Kwa hiyo, Wisconsin huenda ikaenda upande wowote katika uchaguzi ambao wapiga kura waliokaribia kugawanywa kwa usawa wakigawanya maoni ya umma. Katika ushindani wa karibu, pande zote zinajaribu kupata mafanikio na wapiga kura wapya. Kwa Warepublican, hiyo ina maana kujaribu kuingia katika eneo la Wademocrat kihistoria wakiwa ni wapiga kura Weusi, Orlando Owens ni mwenyekiti wa kwanza wa Wamarekani Weusi katika kaunti ya Milwaukee anaeleza haya... - VOA #joebiden #donaldtrump #uchaguziwaawali #Wisconsin #kampeni #wapigakura #watuweusi #voa #voaswahili #scottstearns #afrika